Animation

Blogger templates

FLEVA za katuni kila wakati,Pata sababu ya kutabasamu kila uingiapo!

22 August, 2010


Ifike wakati sasa Watanzania tuwe na msimamo na tusikubali kuchagua viongozi kwa kununuliwa kwani matokeo yake tunapata bora viongozi badala ya viongozi bora.

Kwa kawaida kiongozi aliyechaguliwa kwa kutoa rushwa atakapovurunda, inakuwa ni
vigumu kwa wananchi kumnyooshea vidole, na badala yake wanabakia kulalamikia chini
chini.

Jamani wananchi amkeni uchaguzi wa mwaka huu rushwa isipewe nafasi kamwe haijalishi
ni mgombea wa chama gani, pigieni kura watu mnaoona wanaweza kuwasaidia na kuwatendea haki, tena msikubali kupelekeshwa na watu wachache wanaotaka mchague
watu wanaowataka.

Kura yako inathamani usipoteze kwa mtu ambaye hatakuja kuwa na msaada kwako.http://www.habarileo.co.tz/safu/?n=9332

0 Maoni::